Baada Ya Kukosa Tuzo BET,Chris Brown Amejitetea Kwa Hili

Msanii Chris Brown baada ya kupigwa chini na Bruno Mars kwenye Tuzo za BET ambazo zilifanyika June 24,Kupitia account ya Instagram Chris brown amejitetea,jambo ambalo limeonyesha kuwa amekasirika baada ya kufanya kazi kwa bidii ya kutoa Double Album last Year na bado akakosa tuzo.

Breezy ameandika,"I Don't Need Award To Be A king"(Sihitaji tuzo ili niwe mfalme) ambapo caption hiyo aliifuta baada ya muda mfupi na kuacha picha.
Chris Brown amepitisha miaka mitatu mfululizo bila kushinda tuzo za BET ikiwa 2016,2017 hakushinda na mwaka huu 2018 alitajwa kwenye vipengele viwili Best Male RnB/Pop Artist na Video Director of the year bt hajaibuka mshindi.

 


EmoticonEmoticon