Mtambue Mwanamke Anayekupenda Baada Ya Kumtongoza Hata Kama Hajakujibu

Baadhi ya wanaume wanakuwa katika wakati mgumu sana kwenye mapenzi hasa pale unapomtongoza mwanamke na anachelewa kukurudishia majibu ambayo yanaweza kukupa wewe mwelekeo wa kujua upo upande gani. Baadhi ya wanaume wanaamuaga kukata tama bila kujua mapenzi kwa mwanamke huwa yanajengwa kama nyumba inavyoanzwa na msingi kisha kusimama.

Baadhi ya wanawake/waschana wanahitaji muda ili kuweza kumzoea mwanaume na kujenga kiasi cha upendo moyoni mwake na kuamua kuchukua jukumu la kutoa moyo wake na kumkabidhi, kama tunavyojua mwanamke akipenda basi amependa.
Hii ni fursa kwa wanaume ambao wanakata tama bila kutambua ishara kwa mwanamke ambaye bado hajarudisha majibu baada ya kumtongoza, zijue ishara za mwanamke huyo hapo chini.
Anaongeza ukaribu
Ukiona anapenda kuwa karbu na wewe na kuandamana na wewe na anajisikia ufahari kuwa na wewe jua anaelekea kukukubali. Ukiona anajishauri ujue labda anaona hamlingani kuwa pamoja.
Anaanza kukuchunguza
Ukiona haachi kukuuliza maswali binafsi na kutaka kufahamu unaishije ikiwa na pamoja na kufahamu mambo unayoyapenda mfano unapenda vyakula vipi ujue anapenda kukujua zaidi ili akupendeze.

Anaulizia ndugu zako

Ukiona anapenda kukuulizia habari za ndugu zako na kutaka kuwafahamu basi ujue tayari amekukubali na anaanza maandalizi ya kujenga mahusiano nao.

Anakwambia mambo yake

Ukiona hupenda kukupasha habari zake binafsi na za ndugu zake wakiwemo marafiki zake basi ujue amekukubali na anakuaandaa kuwa kama mwenzake.

Anaonyesha kwa matendo

Kwa mfano anajishikashika maeneo ambayo yanautangaza uzuri wake kama usoni, nywele zake au hata kurekebisha nguo zake jua anajaribu kuwa mtanashati mbele yako ili akuvutie. Katika mazingira hayo dalili zote zipo kuwa kuna uwezekano mkubwa tayari anakukubali.EmoticonEmoticon