#SPORTS: PSG Ipo Tayari Kumuuza Gwiji Wa Brazil Neymar

Hatima ya Neymar katika club ya Paris Saint-Germain inazidi kupigwa darubini baada ya ripoti kuwa mabingwa hao wa ufaransa wako tayari kumruhusu mshambulizi huyo wa Brazil kuondoka katika kipindi hiki cha uhamisho.

Siku ya Jumapili, jarida la L’Equipe liliripoti kuwa PSG watafurahi kukubali ‘Offer kubwa’ ili kumuuza Neymar, ambaye imeripotiwa kuwa hatima yake iko mbali na Parc des Princes.
Staa huyo wa miaka 27 anahusishwa na kurudi klabu ya Barcelona au pia Real Madrid kujiunga na kocha Zinedine Zidane ambaye ameanza kujenga timu hiyo upya.
Maisha ya Neymar ya usoni yamekuwa mada mara kwa mara tangia alipo jiunga na PSG kwa uhamisho ambao ulivunja rekodi wa kitita cha pauni milioni 198, Agosti mwaka wa 2017.
Inasemekana kuwa PSG itachukua zaidi ya kitita walichomsajili nacho ili wakubali kumuuza.
Raia huyo wa Brazili ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa mda mrefu baada ya kuumia mguu katika mechi za matayarisho kabla ya michuano ya Copa America, mapema mwezi huu.
Neymar alifungia PSG mabao 51 katika mechi 58 ambazo alichezea PSG na akawasaidia kunyakua mataji mawili msimu uliopita.


EmoticonEmoticon