
Mara nyingi watu wanaugua maradhi
mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au
kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya
dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka
hayo na kuanza kuzitumia.
Ni ukweli usiopingika kuwa dawa
zimetengenezwa ili kutibu maradhi fulani ambayo yatabainika kwa mgonjwa baada
ya uchunguzi wa kitaalamu.
Hivyo matumizi ya dawa bila kufanya
uchunguzi wa kitaalamu yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya yako

TAZAMA MADHARA 5 HAPO CHINI
1. Huweza kusababbisha kifo.
Kama nilivyoeleza kwenye hoja
zilizotangulia, dawa ni sumu zinazokabili vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia
dawa vibaya kunaweza kusababisha kifo.
Ikumbukwe pia watu wenye matatizo
maalumu kama vile maradhi ya moyo pamoja na shinikizo la damu, wanapaswa kuwa
makini na dawa wanazozitumia kwani zinaweza kuchochea matatizo yao na hatimaye
kifo
2. Huweza kusababisha saratani.
Dawa zinapoingia mwilini mwako kimakosa
na kushindwa kufanya kazi yake, zinaweza kuharibu baadhi ya seli za mwili na
kuzifanya kugeuka seli za saratani. Hivyo hakikisha dawa unayoitumia ni sahihi
na inalenga ugonjwa husika.
3. Husababisha usugu wa maradhi
Mtaalamu wa afya hukupa kiwango
(dosage) cha dawa kulingana na vipimo alivyovifanya; hivyo kutumia dawa bila
vipimo vya kitaalamu kunaweza kusababisha vimelea vya ugonjwa vizoee dawa
husika na kusababisha ugonjwa huo usitibike tena.
Hili ndilo linalosababisha maradhi kama
vile malaria sugu au UTI sugu. Hivyo kabla ya kutumia dawa ni vyema ukafanya
uchunguzi wa kitaalamu
4. Husababisha tatizo la mzio. Allegy.
Kuna watu wenye tatizo la mzio au wengi
huita “aleji” kwa lugha isiyo sanifu, watu hawa wanapaswa kuwa makini na
kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu.
Hili ni kutokana na baadhi ya dawa
kutokuendana na afya zao, hivyo kusababisha tatizo lao la mzio kuibuka. Ni
vyema ukamwona mtaalamu wa afya na umweleze aina ya mzio uliyo nayo ili akupe
dawa stahiki.
5. Huongeza sumu mwilini.
Dawa zimetengenezwa kwa kutumia
kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa.
Hivyo kutumia dawa bila vipimo
kunakusababishia kuongeza sumu za dawa hizo mwilini mwako kwani umetumia dawa
ambazo mwili hauzihitaji kukabili ugonjwa husika.
Sumu hizi zinapokusanyika mwilini mwako
zinaweza kukuletea athari mbalimbali za muda mfupi au hata mrefu.
Ni muhimu ukumbuke kuwa dalili za
ugonjwa mmoja zinaweza kuwa dalili za ugonjwa mwingine pia. Hivyo ni muhimu
kufanya uchunguzi pamoja na kutafuta ushauri wa kitabibu kabla ya kutumia dawa
zozote kutibu maradhi yanayokukabili.
EmoticonEmoticon