Yajue Madhara Ya Unene

Unene kwa sasa umekuwa moja ya kisababishi cha ugonjwa wa saratani nchini Uingereza kuliko uvutaji sigara, taasisi ya saratani nchini humo imeeleza.
Taasisi ya utafiti ya ugonjwa wa saratani imesema, saratani ya ini, utumbo, ovari zinasababishwa kwa kiasi kikubwa na uzito mkubwa kuliko kuvuta tumbaku.
Inasema mamilioni wako hatarini kuugua saratani kwasababu ya uzito na kuwa watu wenye uzito mkubwa huzidi idadi ya wavuta sigara kwa wastani wa watu wawili kwa mmoja.

Lakini taasisi hiyo imesema uzito mkubwa au unene husababisha wagonjwa wa saratani 22,800 kila mwaka, ukilinganisha na uvutaji wa sigara unasababisha watu 54,300 kuugua saratani.

Uhusiano kati ya unene na saratani ni kwa watu wakubwa pekee, ingawa kwa watoto wadogo ni muhimu wachukue tahadhari pia.


EmoticonEmoticon