Kuosha
mikono, nguo na kusafisha sehemu kwa wakati muafaka ndio chanzo cha afya nzuri-
lakini mtu mmoja kati ya wanne wanadhani hilo sio muhimu, ripoti hiyo inaonya.
Kulifanya hilo kwa njia sawa kunaweza kupunguza maambukizi na
magonjwa kukaidi dawa za antibiotic.
kuna
mchanganyiko kwa umma kuhusu utofuati katiya uchafu na viini vya uchafu au
germs, usafina afya.
Katika utafiti wa watu 2,000, asilimia 23 walidhani watoto wanihatji
kushika uchafu ili kujenga mfumo wa kinga mwilini.
Lakini wataalamu katika ripotihiyo wanasema "kuna uwezekano wa
madhara" yanayoweza kuwafanya kupata maambukizi hatari.
Badala yake, walisema watu wanastahili kuangalia usafi wa maeneo
maalum kwa wakati maalum, hata kama maeneo hayo yanaonekana kuwa masafi, ili
kuweza kuzuia kusambaa kwa viini vya uchafu.
Maeneo
Muhimu Yanayohitaji Kusafishwa
§
Maeneo yakupika na
kutayarisha chakula
§
Kula kwa vidole
§
Baada ya kutoka msalani
§
Unapokohoa, kupiga chafya au
kupangusa kamasi
§
Unaposhika au kuosha nguo
chafu
§
unapowashughulikia wanyama
§
unapokusanya au kuondosha
taka taka
§
unapomhudumia jamaa aliye na
kidonda mwilini
Ni
muhimu sana kusafisha mikono baada ya kushughulikia chakula, unapotoka msalani
unapokohoa au unapowashughulikia wanyama nyumbani, ripoti hiyo imesema.
Kusafisha jikoni na vyombo vya kukatia mboga ni muhimu baada ya
kutayarisha vya vyakula vibichi kama mboga na nyama, au kabla ya kutayarisha
chakula.
Vitambaa vya jikoni na brashi zinazotumika kwa usafi ni muhimu
kuzisafisha baada ya matumizi.
Makundi 3 ya
vitu unavyopaswa utumie katika Usafi huo
§
Sabuni - husafisha na kutoa
mafuta lakini haziui bakteria.
§
Dawa za kuuwa vidudu - huua
bakteria lakini hazisafishi vilivyo maeneo yalio na mafuta na uchafu.
§
Dawa za kusafisha - Zinaweza
kutumika kusafisha na kuua bakteria.
Badala ya kutumia kitambaa kusafisha maeneo baada
ya kupika chakula, tumia karatasi. hii husaidia kuepusha vitambaa vinavyotumika
mara kwa mara kubeba uchafu.Ni Muhimu pia kufwata ushauri na maelekezo
ya wataalamu wa Afya.
EmoticonEmoticon