Yajue Madhara Ya Vinywaji Vyenye Sukari

Vinywaji vya sukari ikwemo maji ya matunda vinaweza kuongeza hatari ya saratani , kulingana na mwanasayansi wa Ufaransa.
Uhusiano huo ulifichuliwa na utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu nchini Uingereza , uliwachunguza watu 100,000 kwa kipindi cha miaka mitano.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuiu cha Srbonne Paris Cite wanadai kwamba ongezeko la viwango vya sukari katika damu huenda ndio sababu kuu.

Hatahaivyo utafiti huo haukupata ushahidi kamili na kwamba watafiti wametaka utafiti zaidi kufanywa.

Watafiti wao walisema kwamba ni kinywaji kilicho na zaidi ya asilimia 5 ya sukari. Vinywaji hivyo vinashirikisha maji ya matunda ambayo hayajongezwa sukari,
Vinywaji visivyo na pombe, vinywaji vya kuongeza nguvu, chai na kahawa yenye sukari.
Kundi hilo pia lilichunguza vinywaji visivyo na kalori vinywaji vilivyo na sukari yake lakini hawakubaini uhusiano wowote na saratani.

Utafiti huo pia ulifichua kwamba unywaji wa mililita 100 za ziada za vinywaji vilivyo na sukari kwa siku ikiwa ni chupa mbili kwa wiki kutaongeza hatari ya saratani kwa asilimia 18. Kwa kila watu 100 katika utafiti huo kuna 22 walio na saratani.
Hivyobasi iwapo wote watakunywa mililita 100 kwa siku itasababisha aina nyengine nne za saratani - na kuongeza jumla hiyo kufikia 26 kwa 1000 katika kipindi cha miaka mitano, kulingana na watafiti.
Kati ya visa 2,193 vilivyopatikana wakati wa utafiti huo aina yaaratani 693 zilikuwa zile za matiti , 291 zilikuwa za tezi dume na visa 166 vilikuwa vile vya saratani ya mwisho wa utumbo.

Muungano wa watengenezaji vinywaji visivyo vya sukari nchini Uingereza wanasema kuwa utafiti huo hautoi ushahidi.
Mkurugenzi mkuu Gavin Prtington aliongezera: Vinywaji vyetu ni viko salama na ni miongoni mwa vya lishe bora.
Sekta ya utengezaji wa vinywaji hivi ina jukumu katika kusaidia kukabiliana na kunenepa kupitia kiasi na ndio sababu tumepunguza kiwango cha sukari na kalori.


EmoticonEmoticon