Aina 12 Za Maumivu Ya Kichwa

KUUMWA kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana, inaweza kutokea kwa kusababishwa na mtiririko wa damu kwenda kichwani au matatizo ya misuli ama matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwa na chini ya ubongo ina mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo ina hisia. Kuna aina 12 ya magonjwa ya kichwa kama yafuatayo:

1: Nervous tension headaches:
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo, kuumwa na kichwa pamoja na kukosa usingizi. Tumia vitamin B2 na C au acha matumizi ya sukari kahawa, chakula chenye kukusababishia mzio, misongo ya mawazo na ufanye mazoezi ya kutosha.

2: Cluster headaches
Kichwa kuuma hasa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protini ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.
3: Hangover headaches: Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali hasa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kisogoni au shingoni, kunywa maji mengi na juisi ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na hasa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili.

5: Caffein headaches
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokidogo mpaka utakapoacha kabisa.

6: Sinus headaches
Maumivu haya huanzia upande wa
kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vyakula vyenye vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa nyingine hali hii hutokana na maambukizi.

7: Bilious headaches
Kichwa na macho huuma, wengine huita kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha kila siku lita moja hadi mbili.

8: Hunger headaches
Maumivu ya kichwa ambayo husababishwa na kutokula chakula kwa muda unaotakiwa. Kula chochote ilimradi kiwe na protini au carbohydrates.

9: Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia sana kitu kwa karibu japo saa nyingine inaweza kuwa sababu, lakini chanzo chake hasa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi na kuchoka. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuona mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya kama hali inakutokea ukiwa na hali hiyo.

11: Arthritis headaches: 
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa nyingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu hasa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo, muone mtaalamu wa afya.

12: Hypertension headaches: 
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na hali itaisha bila shaka. Ukiona hali hii muone mtaalamu wa afya akupime presha.


EmoticonEmoticon