Alichokisema Mesut Ozil Baada Ya Kuvamiwa Na Majambazi

Mesut Ozil ametoa taarifa kufuatia kisa cha kudhohofisha ambapo alivamiwa na majambazi wawili jijini London siku ya Alhamisi .
Kanda za CCTV zinamwonyesha Ozil  na mchezaji mwenzake wa Arsenal Sead Kolasinac wakitishiwa na majambazi wawili waliojifunika sura na walioonekana kujihami kwa visu, walipokua wakiendesha gari, huku Kolasinac akijaribu kuminyana nao.
Mke wa Ozil Amine pia alikuwemo ndani ya gari hilo, lakini kwa bahati nzuri hakuna mmoja wao aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho.
Siku ya Ijumaa Ozil alichapisha kwenye twitter picha yake na Kolasinac wakiwa pamoja na kusema kuwa: “Sead, mke wangu, nami tuko salama baada ya kisa cha jana London.
“Asanteni kwa jumbe zenu za kutia moyo.”
Polisi wa Metropolitan wanachunguza shambulizi hilo kwa sasa lililotokea kwenye barabara ya Platts Lane, karibu na Hampstead.
Taarifa iliyotolewa July 26 ilisema: “Polisi waliitwa Platts Lane, NW3, muda mfupi kabla ya saa 5pm Alhamisi, Julai tarehe 25 kwa ripoti ya jaribio la wizi.”Iiliripotiwa kwamba washukiwa waliokuwa kwenye pikipiki walijaribu kumuibia mtu aliyekuwa akiendesha gari.
“Hakuna aliyekamatwa. Uchunguzi unaendelea.”
Ozil na Kolasinac walikua wamerejea kutoka Arsenal kabla kuanza msimu Marekani shambulizi hilo lililopotokea.
Kolasinac pia alichapisha pisha yake na Ozil mapema siku ya Ijumaa akisema kwamba wako salama.
Kolasinac amesifiwa sana kwa ujasiri wake kwa kuminyana na majambazi hao, ingawaje PFA imewaonya wachezaji wa Premier League kutofanya hivyo iwapo jambo kama hilo litawafika.EmoticonEmoticon