#ENEWS:Celebrities Wanaoingiza Mkwanja Mrefu 2019, Forbes Wathibitisha


Julai 11 Forbes imeachia orodha hiyo na kumtaja mwimbaji mwanadada Taylor Swift kama staa ambaye ametengeneza/amelipwa pesa nyingi zaidi kwa mwaka huu (June 2018 - June 2019) Taylor akiingiza kiasi cha ($185M) sawa TZS Bilioni 424.9

Taylor ametengeneza pesa nyingi kupitia ziara yake ya muziki "Reputation Tour" ambayo ilianza May 2018 - November 2018 ikiingiza kiasi cha ($345.7 Million)

Kylie Jenner amefanikiwa kuakamata nafasi ya pili ($170M) huku nafasi 3 amekamata mwanamuziki Kanye West akiingiza kiasi cha ($150M)

Jay-Z ambaye alitajwa kuwa sasa ana utajiri wa Dollar Billion, kwa mwaka huu ameingiza kiasi cha ($81M) na yupo nafasi ya 20 duniani akifungana na mkewe Beyonce Knowles

Kim Kardashian mke wa Kanye West yupo namba 26 akiingiza kiasi cha ($72M), Diddy yupo namba 28 na kiasi ($70M) kibindoni kwa mwaka 2019.

Wengine ni Rihanna ambaye alitajwa kama msanii wa Kike tajiri zaidi duniani, yupo namba 36 akiingiza ($62M).


Mwaka jana orodha hii iliongozwa na Bondia Floyd Mayweather ambaye mwaka huu hayupo kabisa kwenye watu 100.

FORBES HIGHEST PAID CELEBRITY 2019(TOP 10)

1. Taylor Swift ($185M)
2. Kylie Jenner ($170M)
3. Kanye West ($150M)
4. Lionel Messi ($127M)
5. Ed Sheeran ($110M)
6. Cristiano Ronaldo ($109M)
7. Neymar ($105M)
8. The Eagles ($100M)
9. Dr. Phil McGraw ($95M)
10. Canelo Alvarez ($94M)


EmoticonEmoticon