#ENEWS:Ujio Mpya Wa Beyonce Waijumuisha Afrika Na Lugha Ya Kiswahili

Spirit ni moja kati ya wimbo unaopatikana kwenye albamu inayosindikiza filamu mpya ya Lion King inayotengenezwa na kampuni kubwa ya Disney ya nchini Marekani.

Spirit imeimbwa na mwanamama Beyonce ambaye ni mke wa Rapa Jay-z na ndani yake kuna lugha ya kiswahili inasikika mwanzo wimbo huo unapoanza, "Uishi kwa muda mrefu mfalme.."

Filamu ya Lion King, "inajumuisha sauti za kutoka barani Afrika," imeeleza kampuni ya Disney.

Kampuni hiyo inasema kuwa albamu hiyo iitwayo The Lion King: The Gift, itaachiliwa tarehe 19 mwezi wa 7.

SIKILIZA HAPA


EmoticonEmoticon