Fahamu Kioo Ambacho Kinakusaidia Kwenye Make Up (Kujiremba Uso)


Umeshawahi kumuona mtu aliyejiweka ‘make Up’ usoni tena kwa kutumia kioo na akawa kichekesho kwa wengi? Aidha kwa kujiweka poda zilizopita kiasi au kuonekana kama mwenye ngozi iliyochafuliwa badala ya kupambika? Smart Beauty Mirror ni msaada kwa wadada walimbwende.

Basi kwa wale ambao wameshawahi kukutana na kadhia hiyo, wameletewa suluhisho kwa kioo Janja (Smart Mirror) kinachofahamika kama Smart Beauty Mirror kilichobuniwa na Kampuni ya HiMirror ambao ni wataalamu masuala ya ngozi na mwili.
Kwa wale wenye kupenda masuala ya ulimwende wa sura zao na kujikagua kabla ya kutoka basi
kioo janja hiki ni ajili yao kitakachowasaidia kazi ya kijiremba kuwa urahisi na uhakika zaidi.
1. Kioo hiki kina kamera ambayo hutathmini kila sehemu ya ngozi yako hususani kwenye uso.

2.Kitakuonesha ikiwa ngozi imejikunja, imeparara, hujapaka mafuta vizuri au ikiwa kuna kovu ambalo huenda likakuharibia muonekano wako mzuri.

3.Pia kitakushauri namna ya kuuremba uso wako kulingana na wakati gani. Kama ni Make Up kwa ajili ya muda wa Asubuhi, mchana, Jioni au usiku.

4.Kadhalika, hukufahamisha ikiwa ngozi yako ina matatizo ya kiafya na kukushauri kumwona daktari.

Kioo Janja hiki kilianza kuuzwa Jualai 2018 tayari kinapatikana kuuzwa kupitia mtandao wa Amazon kwa kiasi cha Dola za Marekani 149 ambazo ni sawa na Tshs 343,000/-


EmoticonEmoticon