Katy Perry Akutwa Na Hatia Ya Kucopy Wimbo Usio Wake

Katy Perry amekutwa na hatia ya kutokuwa na hatimiliki ya ngoma ‘Dark Horse’ ambayo ilidaiwa kuwa iliigwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya BBC imeeleza kuwa Jumatatu Julai 29,2019 Mahakama mjini New York imethibitisha kuwa wimbo huo wa ‘Dark Horse’ uliotoka rasmi mwaka 2013 uliigwa  kutoka kwenye wimbo wa ‘Joyful Noise’ ulioimbwa na mwimbaji anayetumia jina la Gospel, 'Flame' jukwaani mwaka 2011 huku jina lake halisi akiitwa Marcus Gray.Pamoja na kukutwa na hatia hiyo mtayarishaji nyimbo wa Katy Perry, 'Dr Luke' aliiambia mahakama kuwa hakuwahi kusikia wimbo wa ‘Joyful’ uliotoka mwaka 2009.
Katika utetezi wake, Perry alisema anaweza kuimba wimbo wake ‘Live’ mbele ya mahakama lakini ilishindikana kutokana na wakili wake kupata hitilafu ya vifaa na kushindwa kucheza ngoma ya ‘Dark Horse’.
Rapa Juicy J & Katty Perry (Picha By Getty Images)

BBC imeeleza mahakama imewatia hatiani watu sita akiwemo mwandaaji wa nyimbo mtunzi wa nyimbo Sarah Hudson na Juicy J na kuelezwa kuwa itawekwa wazi kiasi atakachotakiwa kulipa Katty Perry kwa Marcus Gray, kutokana na kunakili wimbo huo.


EmoticonEmoticon