Kesi Ya Ronaldo Unyanyasaji Wa Kingono

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo hatakabiliwa na shtaka lolote baada ya kutuhumiwa na madai ya unyanyasaji wa kingono, waendesha mashtaka wa Marekani wamesema.
Kathryn Mayorga, 34, alidai kuwa mchezaji huyo wa klabu ya Juventus alimbaka katika hoteli moja mjini Las Vegas mwaka 2009.
Iliripotiwa kuwa Bi Mayorga alikubaliana na nyota huyo kusuluhisha kesi hiyo kimya kimya nje ya mahakama mwaka 2010.
Lakini aliamua kufungua tena kesi hiyo mwaka 2018, baada ya Ronaldo kupinga madai hayo.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, waendesha mashitaka wa Las Vegas walisema madai hayo hayakuweza kutibitishwa.
"Hakuna shitaka litakalotolewa," taarifa hiyo ilisema.
Gazeti la kila wiki la Ujerumani Der Spiegel, lilichapisha taarifa kuhusu madai hayo mwaka jana.
Gazeti hilo liliandika kuwa Bi. Mayorga alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya tukio hilo.
Mwaka mmoja baadae, ripoti ilitolewa ikimhusu Ronaldo kukubali kutoa kitita cha dola milioni 375,000 ili kesi hiyo imalizike kimya kimya bila kutoa taarifa kwa umma kwa kulinda heshima yake.
Uamuzi wa wanasheria wa Bi Mayorga kuvunja kimya chao kuhusu unyanyasaji huo wa kingono ulitokana na kampeini ya #MeToo movement.


EmoticonEmoticon