La Liga Itaweza Kuzuia Usajili Wa Antoine Griezmann kutoka Barcelona kwenda Atletico Madrid

Usajili wa Antoine Griezmann kwenda Barcelona unaweza kuzuiwa kutokana na mzozo wa malipo.
Uwezekano wa kutokea hatua hiyo umedokezwa na Raisi wa ligi kuu ya Uhispania maarufu La Liga, Javier Tebas.
Klabu aliyotoka Griezmann, Atletico Madrid ilituma malalamiko baada ya Barcelona kutangaza kumsajili Griezmann kwa kukubali kutoa kitita cha euro milioni 120 kama matakwa ya mkataba wa mchezaji huyo ulivyoainisha mnamo Julai 12.
Bei ya mchezaji huyo kimkataba ilishuka kutoka euro milioni 200 mpaka milioni 120 ilipotimu Julai Mosi.


EmoticonEmoticon