Kama unahisi
kichefuchefu, tumbo linasokota, linafura, lina gesi, au unaharisha baada ya
kunywa maziwa au kula vyakula vinavyotengenezwa na maziwa, elewa kuwa una
ugonjwa unaosababishwa na maziwa kitaalamu huitwa lactose
intolerance.
Mtoto
mchanga akiathiriwa na maziwa na kukutwa na dalili hizo hapo juu, yeye pamoja
na wazazi wake wanaweza kutatizika sana. Mtoto akianza kuharisha, anaweza kuishiwa
maji mwilini. Iwapo itagunduliwa kwamba anaathiriwa na maziwa, iwe ya mama, ya
ng’ombe au ya unga, madaktari hupendekeza apewe vyakula vingine badala ya
maziwa.
Wengi wamepata nafuu baada ya kufuata mapendekezo hayo.
Ugonjwa huo huwapata baadhi ya watu na watoto
wanapotumia maziwa na bidhaa za maziwa. Kulingana na kitabu The Sensitive Gut,
kilichochapishwa na Shule ya Kitiba ya Harvard, imekadiriwa kwamba karibu
asilimia 70 ya watu ulimwenguni huathiriwa kiafya na maziwa.
Laktosi ni sukari inayopatikana katika
maziwa. Utumbo mdogo hutoa kimeng’enya kinachoitwa lactase, ambacho huvunja
laktosi ili iwe glukosi na galactose. Sasa damu inaweza kuitumia sukari hiyo.
Lakini ikiwa hakuna kimeng’enya cha kutosha, laktosi huingia katika utumbo
mkubwa bila kuvunjwa kisha huanza kuchacha na kutokeza asidi na gesi.
Dalili za
ugonjwa ni kufura kwa tumbo, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na kutapika.
Kimeng’enya cha lactase hutengenezwa kwa
wingi mtu anapokuwa mtoto wa miaka miwili, kisha baada ya hapo huanza kupungua.
Watu wengi hufikiri kwamba wana mzio wa maziwa wanapougua magonjwa
yanayosababishwa na maziwa.
Kwa ujumla, mizio ya chakula si mingi, na ni
asilimia moja mpaka mbili ambao huathiriwa. Watoto wengi zaidi huathiriwa
ingawa hawazidi asilimia nane. Dalili za mizio na za magonjwa ya maziwa
zinaweza kufanana, lakini kuna tofauti chache. Mzio hutokea wakati mwili
unapokuwa ukijikinga na kitu kibaya ambacho umekula au kunywa. Mwili hutokeza
kemikali inayoitwa histamine.
Dalili nyingine za mzio zinaweza kuwa kufura
mdomo au ulimi, vipele, au pumu. Dalili hizo hazitokei mtu anapougua ugonjwa
unaosababishwa na maziwa kwa sababu kinga ya mwili haihusiki. Badala yake mtu
huwa mgonjwa kwa sababu tumbo hushindwa kusaga chakula vizuri.
Lakini ikiwa ana mzio, kuna sababu ya
kuhangaika. Madaktari wengine huwapa dawa ya kuzuia histamine. Hata hivyo,
ikiwa anashindwa kupumua, daktari atahitaji kufanya mengi zaidi ili kuzuia hali
hiyo. Mtoto akianza kutapika, huenda ana ugonjwa mwingine unaoitwa galactosemia
ambao hutokea mara chache.
Kama tulivyotaja mapema, lactase hutokeza sukari ya
galactose,ambayo pia huhitaji hubadilishwa iwe glukosi.
Sukari ya galactose ikirundamana mwilini,
inaweza kuharibu ini, figo, kupungukiwa na akili, kupata ugonjwa wa
hypoglycemia, na hata mtoto wa jicho (cataract).
Hivyo ni muhimu kuacha kabisa
kumpa mtoto maziwa au bidhaa za maziwa mapema ikiwa ataonyesha dalili tajwa
hapo juu.
Kwa sasa hakuna matibabu yanayoweza kumsaidia
mgonjwa atokomeze kimeng’enya cha lactase. Hata hivyo, kwa kawaida magonjwa
yanayosababishwa na maziwa hayasababishi kifo.
MATIBABU
NA KINGA
Wengine wameamua kutotumia bidhaa za maziwa
hata kidogo baada ya kuona matatizo wakiyatumia.
Wale wanaotaka kuendelea kutumia bidhaa za
maziwa wanaweza kwenda kwa daktari na akawaandikia dawa ambazo zina lactase ili
kusaidia matumbo kuvunjavunja laktosi. Dawa hizo zinaweza kumsaidia mtu
asiathiriwe na maziwa.
EmoticonEmoticon