Man U Wakataa Kumuuza Mchezaji Huyu Kwa Dau Nono

Manchester United wamekataa dau pauni milioni 53.9 kutoka kwa Inter Milan walizotaka kuzitoa kumnunu mshambuliaji wake Romelu Lukaku.
Dau hilo ni chini ya thamani ambayo Manchester united imempa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26- raia na mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Belgiumaliyejiunga nao kutoka Everton miaka miwili iliyopita kwa pauni milioni 75.
Meneja wa Inter Milan Antonio Conte amemfanya Lukaku - ambaye hatacheza katika kikosi cha United dhidi ya Italia nchini Singapore Jumamosi - mchezaji nambari moja anayelenga kumnunua.
"Wafahamu , ninmpenda mchezaji huyu ," alisema Conte Ijumaa.
" Nilipokuwa kocha wa Chelsea, nilijaribu kumleta Chelsea.
"Ninampenda mchezaji huyu, na ninamchukulia kama mchezaji muhimu kwetu ili kuweza kupata mafanikio, lakini wakati huo huo kuna soko la uhamisho.
"tutaona kitakachotokea -lakini kwa sasa Lukaku ni mchezaji wa United ."
Hatua ya Inter Milan ya kumtaka Lukaku inaonyesha kumaliza azma ya Mauro Icardi, ambaye hajasafiri katika safari ya msimu huu katika kikosi hicho ya Asia huku kukiwa na ripoti kuwa ataondoka.
Alipoulizwa kuhusu mshambuliaji wa Argentina , Conte alijibu : "klabu iko wazi kwamba Icardi yuko nje ya mradi wa Inter Milan. Hii ndio hali halisi ."
Aliposhinikizwa na swali kuhusu hali ya baadae ya Lukaku katika Ijumaa wiki hii , Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alisema kuwa "sina taarifa mpya".
Mbelgiji huyo alikosa ,mechi zote za Machester United ilipocheza nchini Australia kutokana na majera
"Hayuko fiti. Hatakuwepo,"alisema Solskjaer.


EmoticonEmoticon