Manchester City Hawataki Kumuuza Sane

Pep Guardiola anasema anamtaka Leroy Sane kusalia Manchester City lakini anakiri kuwa uamuzi huo si wake.
Sane ana miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wake lakini hajasema lolote kuhusu majadiliano ya kuuongeza mkataba.
Bayern Munich inataka kumsajili Sane. Bayern ilifanya majadiliano na wawakilishi wa Sane mapema wiki hii kuhusiana na uwezekano wa uhamisho Allianz Arena.
City hawataki kumuuza Sane na bado hawajapokea ofa rasmi kwa ajili ya wing’a huyo Mjerumani.


EmoticonEmoticon