Yajue Haya Muhimu Kabla Ya Kuingia Kwenye Ndoa

Ni vizuri ukaiandaa akili yako kabla haujafanya maamuzi sahihi yatakayopelekea maisha yako kuwa na furaha au kilio hapo baadaye kwa yule uliyemchagua kuwa naye.

Ila tabia na mambo hayo hapo chini huwa yanabadilika kuendana na wakati na sio kila binadamu hawezi kubadilika kitabia, wapo wanaoweza kubadilika pia.

YAJUE HAYA
1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.

2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada
ya Ndoa.(Inategemeana na mtu pia ila sio kwa wote)

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu
yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi
fanywa na mtu yeyote.

5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na
Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama
kuolewa na mtu hasiye sahihi.

7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.(Katika hili pia sio wote ambao ni wa kuepukwa wengine ni mapungufu yao na wakipata ushauri mzuri hubadilika)

8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe
na Ndoa yenye furaha.

9. Maneno matatu yanayojenga amani katika
Ndoa:
a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante.

10. Kupiga punyeto ni kujiharibu.

11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga
bila jua.

12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
Mungu mmoja - Mume mmoja - Mke mmoja.

13. Furaha ya kudumu maisha hutegemea na
chaguo lako la Ndoa.

14. Usioe pesa au mali - muoe mtu.

15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa
isiyo na amani na furaha.

16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano
mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke
mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama
kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa kigezo
tu anakidhi haja zako kingono.

18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki
wema.

19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.

20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza…

MUHIMU.Zingatia haya na utapata furaha na amani katika ndoa yako baada ya kufanya maamuzi na chaguo sahihi la yule utakayekwenda kuishi naye.


EmoticonEmoticon