Meek Mill Amaliza Kifungo Kilichokuwa kinamkabili Toka 2008.

Meek Mill amemalizana na jinamizi la miaka 11, ni kile kifungo cha nje (Probation) ambacho amekuwa nacho tangu akamatwe kwa kosa la dawa za kulevya na kumiliki silaha mwaka 2008.
Mahakama ya Pennsylvania mapema July 24 imempatia Meek Mill ushindi huo mkubwa wa kufutwa kwa hukumu yake ulioambatana na maamuzi ya Kusikilizwa Upya kwa kesi hiyo (New Trial) ambapo majaji watatu wamefanya maamuzi hayo bila kupingwa.

Hukumu ya Jaji Genece Brinkley ya November 6, 2017 ilimhukumu Meek Mill kifungo cha Miaka 2-4 Jela kwa kuvunja masharti ya muda wa Uangalizi (Probation) kiasi cha kupelekea dunia kulipuka kwa pingamizi.


EmoticonEmoticon