Meek Mill Aungana Na Jay-Z kufungua Record Label Mpya (PICHA)

Meek Mill ameshirikiana na Jay-Z kuanzisha Label yake iitwayo (Dream Chasers Records) ndani ya mwamvuli wa Roc Nation. Wawili hao wamesaini makubaliano hayo jana Jumanne mjini New York katika makao makuu ya Roc Nation.
Akibaki kama Rais wa Dream Chasers ambayo sasa itashirikiana na kampuni ya Roc Nation ya Jay-Z, Meek Mill atakuwa mfuatiliaji mkuu wa Label hiyo na kutengeneza mfumo wa wafanyakazi vile vile kusaini na kuwaendeleza wasanii. 
Pia Dream Chasers itasimamia shughuli zake yenyewe, mikakati ya kibunifu, masoko na mahusiano ya biashara.

Meek Mill pia amepanga kufungua Studio ya kurekodi kwa ajili ya kutumiwa na wasanii wa Label yake. 
Jay-Z ambaye amekuwa na Roc Nation kwa miaka 11 sasa amesema, kuwa na Meek Mill kama mteja wake kwenye masuala ya menejimenti ni kitu kikubwa sana kwa sababu tayari amekomaa kwa ambayo ameyafanya hadi sasa. Hivyo anaamini ataongoza vyema jahazi la kizazi kijacho.


EmoticonEmoticon