Nicolas Pepe Ndani Ya Arsenal?

Nicolas Pepe ameonekana katika video akiwa amevaa jezi ya klabu yake mpya ya Arsenal.
Mshambuliaji huyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali katika kikosi hicho baada ya kuikamua Arsenal Pauni72 milioni akitokea Lille ya Ufaransa.
Pepe amevunja rekodi ya Pierre-Emerick Aubameyang aliyetua Arsenal kwa Pauni 56 milioni akitokea Borussia Dortmund.
Taarifa za ndani zimedokeza kuwa winga huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24 alikutana na maofisa wa klabu hiyo ya Emirates.
Picha zilimuonyesha akiondoka katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo na nyingine akiwa amevaa jezi ya Arsenal. Winga huyo amefunga mabao 35 katika mechi 74 alizoicheza Lille tangu mwaka 2017.
Usajili wa Pepe uligubikwa na utata baada ya klabu hiyo kusita kutoa Pauni72 milioni ilizotaka Lille.


EmoticonEmoticon