Real Madrid Wazuia Gareth Bale Kuondoka Klabuni Hapo

Uhamisho wa winga wa Real Madrid kuelekea China umefutiliwa mbali na sasa winga huyo wa Wales anatarajiwa kusalia Real Madrid
Bale, 30, alitarajiwa kujiunga na klabu ya China Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kulipwa £1m kwa wiki .
Wiki iliopita mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane alisema kuwa Bale alikuwa anakaribiakuondoka Madrid baada ya kiwango chake cha mchezo kuzorota.
Zidane aliongezea kwamba kuondoka kwake kutakuwa vyema kwa kila mtu. Bale alijiunga na miamba hiyo ya Uhispania kwa dau lililovunja rekodi la £85m kutoka Tottenham 2013.


EmoticonEmoticon