#SPORTS:Algeria Waibuka Washindi AFCON 2019

Algeria imeshinda kombe la mataifa ya Africa kwa mara ya pili baada ya kujipatia goli la mapema panapo Dk2 dhidi ya Senegal katika fainali iliochezwa mjini cairo.
Shambulio la Baghdad Bounedjah lilimgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kupita juu ya mlinda langgo Alfred Gomis
Senegal, ambao hajawahi kushinda michuano hiyo , walipewa penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira katika kipindi cha pili lakini refa wa video VAR alibadilisha uamuzi huo na kusema penalti haikufaa kutolewa.
Algeria ilitumia kila mbinu kuwazuia wachezaji wa Senegal waliofanya mashambulizi ya kila aina ili kushinda kombe hilo tangu 1990.
Senegal ambao walikuwa wakishiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002 , walitawala kipindi kikubwa cha mechi lakini wakashindwa kuzalisha matunda


EmoticonEmoticon