#SPORTS:Algeria Yatinga Nusu Fainali Afcon 2019

Timu ya taifa ya Algeria almaarufu kama ‘The Desert Foxes’ ilijikatia tiketi ya kuingia nusu fainali baada ya kuicharaza Ivory Coast. 
Sofiane  Feghouli aliweka Algeria kifua mbele mnamo dakika ya 20.
Baghdad Bounedjah alikosa kuwaamsha mashabiki wa Algeria mnamo dakika ya 48 alipopoteza mkwajuwa wa Penalti
Jonathan Kodjia alisawazishia Ivory Coast. Mechi hii ililazimika kuamuliwa kwa njia ya penalti baada ya sare ya 1-1. 
Wilfred Bony alipoteza mkwaju wake huku Serey Die akipiga mlingoti hivyo kuipa Algeria ushindi.
Kwingineko ni kuwa Tunisia ilicharaza Madagascar 3-0 na kupenya nusu fainali ya pili. 
Ferjani Sassi aliweka Tunisia Uongozini kabla ya Youssef Msakini kuongeza goli la pili dakika ya 60. 
Naim sliti alitia msumari wa mwisho kwenye ndege ya kuwarudisha madagascar nyumbani kwao kunako dakika ya 90.
Kufuatia matokeo hayo sasa Algeria itamenyana na Nigeria kwenye nusu fainali ya kwanza huku Senegal ikichuana na Tunisia kwenye nusu fainali ya pili. 
Mechi hizi za nusu fainali zitachezwa tarehe kumi na nne mwezi julai.


EmoticonEmoticon