#SPORTS:Arsenal Kuwasajili Wachezaji Nyota Na Ghali Zaidi

Arsenal inajaribu kuwasajili wachezaji maarufu walio ghali zaidi msimu huu kulingana na mkufunzi Unai Emery.
Baadhi ya makundi ya mashabiki na wanablogu wametaka kuwepo kwa mabadiliko katika klabu hiyo na Emery amesema kuwa The Gunner inatafuta wachezaji wenye haiba ya juu katika uhamisho wao.
Tayari maombi yao ya kutaka kumnunua winga wa Cryastal Palace Wilfried Zaha na beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney yamekataliwa.
''Lengo letu ni kuwasajili wachezaji watatu au wanne ambao wataimarisha timu yetu pampoja na kikosi chetu'', alisema Emery.
''Tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kutusaidia na kusonga mbele. Kuna wachezaji wengine ambao wanaweza kuja ili kutusaidia. Tunatafuta wachezaji wazuri sana na sasa tunazungumzia kuhusu uwezekano wa kuwasajili wachezaji maarufu na walio ghali''.
Kufikia sasa ni mchezaji raia wa Brazil Gabriel Martinelli aliyesajiliwa lakini pia wanamlenga beki wa Saint Etiene William Saliba-ijpokuwa wapizani wao wa London kaskazini Tottenham pia nao wanamnyatia raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18.
Bada ya kushindwa kufuzu katika mechi za mabingwa Ulaya , bajeti ya Arsenal imedaiwa kuwa £40m.
Kufikia sasa wamewasilisha ofa ya £25m kumnunua mchezaji wa Uskochi Tierney pamoja na £40m kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast na Crystal Palace Zaha ambaye amesalia na miaka 4 katika kandarasi yake na anadaiwa kuwa na thamani ya £80m na Palace.
''Sidhani kwamba Arsenal wamewasilisha ombi ambalo limekaribia thamani yetu'', alisema mkufunzi wa Palace Roy Hodgson.
''Nina hakika kwamba mchezaji amegundua kwamba iwapo kuna mtu ambaye atamchukua kutoka klabu hiyo atataraji kwamba klabu hiyo italipa thamani ya soko ya mchezaji huyo. Hadi mtu atakapofanya hivyo huwa hakuna kikubwa cha kujadiliwa kuhusu Wilfried''.


EmoticonEmoticon