#SPORTS:Arsenal Waimendea Saini Ya Everton Soares Wa Brazil

Arsenal imeonyesha nia ya kuitaka saini ya mshambuliaji wa Gremio, Everton Soares kwa mujibu wa Sky sources.
Mshambuliaji huyo wa Brazil amesema kuwa amepanda ndege, lakini hakusema ni wapi anakwenda katika klabu ipo.
Inafahamika kuwa Arsenal inamtaka Everton kama mbadala wa kukwepa gharama za kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha.
Everton ni mfungaji bora wa Grermio katika msimu uliopita akiwa amefunga mabao 10 katika mechi 28, pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya Copa Amerika akisaidia Brazil kushinda 3-1 dhidi ya Peru katika fainali.
Arsenal inategemea kupata ushindani mkali kutoka kwa Atletico Madrid, ambayo imesema ipo tayari kutoa pauni 30.5milioni kwa ajili ya nyota huyo mwenye miaka 22.
Kocha wa Unai Emery tayari amemsajili chipukizi Gabriel Martinelli (18), lakini Arsenal inaendelea kusaka saini ya beki wa Celtic, Kieran Tierney pamoja na beki wa Saint Etienne, William Saliba.


EmoticonEmoticon