#SPORTS:Benin, Senegal Zatimba Robo Fainali AFCON 2019

Benin iliichapa Morocco mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penati na kujikatia tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mama Seibou ndiye aliyeweka kimyani penati ya ushindi na kuisogeza mbele timu ya Benin iliyokuwa na wachezaji 10 baada ya Khaled Adenon kutolewa uwanjani katika muda wa ziada wa mchezo huo.
Uganda imeondolewa katika mashindano hayo lakini wachezaji wake waliiweka taifa hilo mbele kwa kuonesha mchezo mzuri na pea talata ya wachezaji wake.
Senegal imeondoa timu zote za Afrika Mashariki ambapo ilianza na Tanzania, Kenya na sasa Uganda.
Sadio Mane ndiye aliyeisaidia Senegal kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuilaza Uganda bao 1-0.
Benin ambao wanashiriki kwa mara ya nne mashindano ya Afcon sasa watakipiga na Senegal katika awamu ya ribo fainali itakayochezwa Julai 10.


EmoticonEmoticon