#SPORTS:Etii Sarri Aliisaliti Timu Hii Kabla Ya Kusaini Juventus

Mshambulizi wa Napoli, 'Lorenzo Insigne' amesema kuwa aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo maurizio sarri alisaliti klabu ya Napoli kwa kukubali kujiunga na klabu ya Juventus.
Sarri alikuwa mkufunzi wa Napoli kwa misimu mitatu huku katika misimu yote akimaliza katika nafasi ya pili huku Juventus ikitwaa taji nyakati hizo zote.
Kwa sasa, Sarri ndiye mkufunzi mpya wa Juventus baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka mitatu. Insigne kwa sasa ndiye nahodha wa Napoli. Alitia mkataba wa miaka minne msimu uliopita huku akisema kuwa matamanio yake ni kustaafu soka akikipigia Napoli.


EmoticonEmoticon