#SPORTS:Jose Morinho Apiga Chini Dili LA China

Jose Mourinho amekataa ofa ya kwenda kufundisha nchini China.
Mourinho amehusishwa na taarifa za kufuatwa na timu ya Guangzhou Evergrande akipewa ofa ya kitita cha pauni milioni 88.
Donge hilo lingemfanya kuwa kocha anayelipwa fedha nyingi duniani lakini Mourinho ametaka kuendelea kubaki Uingereza na familia yake.
Mourinho hajawa kazini tangu alipofukuzwa na Manchester United mwaka jana mwezi Disemba.
Guangzhou kwa sasa wanafundishwa na kocha muitaliano Fabio Cannavaro.
Mourinho alisema mwezi Machi kuwa anataka kurejea kwenye kazi yake ya ukocha mwakaa huu, lakini anasubiri kazi itakayomfaa.
''Ninajua kwa hakika nisichokitaka,'' alisema.
''Ninajua ninachokitaka, si timu fulani lakini namna ya kazi ilivyo na ukubwa wa kazi.''


EmoticonEmoticon