#SPORTS:Kia Joorabchian Aishutumu Klabu Ya Barcelona

Kia Joorabchian wakala wa Philippe Coutinho, ameishutumu klabu ya Barcelona kwa kufanya mpango wa siri wa kubadilishana mchezaji wake pamoja na Neymar na dau la pesa na klabu ya PSG licha ya kuhakikishiwa kwamba mteja wake haendi popote.
Joorbachian amedai kwamba viongozi wa Barcelona ni vigeugeu na wamekuwa katika mpango wa siri wa kumpeleka Coutinho PSG pamoja na dau la pesa ili kumrudisha Neymar Nou Camp katika dirisha hili la uhamisho, kitu ambacho yeye amekishtukia.
Coutinho amekuwa na wakati mgumu Barcelona tangu alipotua klabuni hapo Januari mwaka jana akitokea Liverpool kwa dau la Pauni 140 milioni na amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo huku Barcelona ikiwa imeshamnunua kiungo, Frenkie de Jong katika nafasi yake.
Tangu Neymar aliposema anataka kuondoka PSG, Barca inakomaa kumsajili.


EmoticonEmoticon