#SPORTS:Kocha Frank Lampard Afunguka Baada Ya Sare Ya Chelsea


Kocha wa Chelsea Frank Lampard amekiri kuanza hovyo kwenye maisha yake mapya katika kikosi cha Chelsea baada ya kuambulia sare mbele ya Bohemians katika mechi yake ya kwanza kuiongoza timu hiyo iliyokuwa ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya.
Chelsea walitoka sare ya 1-1 huko Dublin Jumatano usiku, Michy Batshuayi akiipigia The Blues bao la kuongoza kwenye kipindi cha kwanza kabla ya Eric Molloy kuchomoa dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.
Mechi hiyo, kikosi cha Chelsea kilikuwa na sura kibao za wachezaji wenye majina makubwa ambao Batshuayi, viungo Danny Drinkwater na Tiemoue Bakayoko walianzishwa na kocha Lampard, ambaye alichezeshwa vikosi viwili tofauti katika kila kipindi katika mchezo huo.
Baada ya sare hiyo, Lampard, ambaye anahesabika huko Stamford Bridge kuwa gwiji, amesema ana changamoto mkubwa inayomkabili kwenye kikosi hicho.
Alisema: "Ulikuwa mwenendo mzuri, tulipata sapoti kubwa shukrani sana watu wote mliojitokeza. Lakini, ilikuwa mechi ya kwanza ngumu kwetu kwa sababu hatukuwa pamoja kwa muda mrefu.
"Tumekuwa pamoja kwa siku chache sana na wachezaji wamekuwa na presha kubwa kufanya kazi. Nimefurahia matokeo. Ufiti ulikuwa ishu, lakini nilitaka wasumbua kidogo, kuwafanya kuwa kwenye presha. Hizi ni mechi tu za kujiandaa na msimu mpya, punde tutakuwa kwenye ubora tunaotaka. Tulitaka kushinda mechi kama ilivyo kawaida yetu, lakini haikuwa hivyo."


EmoticonEmoticon