#SPORTS:Laurent Koscielny Akataa Kujiunga Na Kikosi Cha Arsenali

Nahodha wa Arsenal Laurent Koscielny amekataa kujiunga na kikosi cha Arsenali kwa mechi za maandalizi ya msimu mpya mjini Los Angeles nchini Marekani.

“Tumesikitika sana na matendo ya koscielny ambayo ni kinyume na matarajio yetu pamoja na maagizo ya klabu. Tunatarajia kusuluhisha jambo hili haraka iwezekanavyo,” Arsenal imesema.

Arsenal inatarajiwa kung’o nanga hii leo kuelekea Marekani ambapo itachuana na Colorado Rapids, Bayern Munich,Fiorentina pamoja na Real Madrid.


EmoticonEmoticon