#SPORTS:Manchester United Yapandisha Bei Ya Pogba

Man U imeripotiwa kupandisha bei ya kiungo wao Paul Pogba baada ya kuona wakala Mino Raiola analazimisha dili la mchezaji huyo kuhamia Real Madrid.
Mino Raiola alifichua wiki iliyopita anafanyia kazi uhamisho wa staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa ili aondoke baada ya yeye mwenyewe kusema anahitaji changamoto mpya nje ya Old Trafford.
Lakini, Man United wameamua kuweka ngumu zaidi baada ya kupandisha bei ya mchezaji huyo kutoka kiwango cha Pauni 150 milioni walichokuwa wakimuuza awali.
Wababe hao wa Old Trafford sasa wanahitaji pesa inayokaribia Pauni 200 milioni ili kuvunja kabisa rekodi ya dunia kwenye uhamisho inayoshikiliwa na staa wa Kibrazili, Neymar ambaye alisajiliwa kwa Pauni 198 milioni miaka miwili iliyopita akitokea Barcelona kwenda Paris Saint-Germain.
Juventus nao wamekuwa wakitajwa kumtaka kiungo huyo.


EmoticonEmoticon