#SPORTS:Matthijs de Ligt Kukamilisha Uhamisho Wake Na Juventus

Nahodha wa mabingwa wa Uholanzi, klabu ya Ajax Matthijs de Ligt yupo safarini kuelekea mji wa Turin Italia kukamilisha uhamisho wake na miamba ya Italia Juventus.
Inaaminika kuwa Juventus watalipa kitita cha pauni milioni 67.5 kwa mlinzi huyo stadi mwenye miaka 19 ambaye aliiongoza Ajax mpaka kwenye nusu fainali za za Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita ambapo walifungwa na Tottenham.
Beki huyo wa kati wa Uholanzi pia alikuwa akihusishwa na kuhamia klabu za Manchester United, Barcelona na Paris-St Germain.


EmoticonEmoticon