#SPORTS:Pogba Hauyupo Mazoezini, Jua Chanzo.

Paul Pogba bado hajaonekana kwenye mazoezi ya Manchester United yaliyoanza Jumatatu wiki hii.

Wakati mastaa wengine wa timu hiyo wakirudi kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya, Pogba amekuwa haonekani huko Carrington kwenye uwanja wa mazoezi, huku ikidaiwa ni kwa ruhusa ya kocha Ole Gunnar Solskjaer - akiwa amemwongezea muda wa kumpumzika mchezaji huyo baada ya miezi 16 ya pilikapilika.

Taarifa kutoka Man United zinadai kwamba kiungo huyo atakuwapo kwenye ndege wakati watakaposafiri kuelekea Australia watakapokwenda kucheza mechi ya kirafiki huko Perth ikiwa ni sehemu ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya.

Pogba na wachezaji wengine Marcus Rashford na David de Gea, walicheza mechi 47 klabuni hapo msimu uliopita, wakiwa ndio wachezaji wa Man United waliocheza mechi nyingi zaidi, kwa mujibu wa BBC Sport.

Na kwamba Rashford na De Gea nao wamepewa siku za nyongeza za mapumziko, huku Pogba akielezwa kwamba aliendelea kutumika kwa mechi za kimataifa alipokuwa akiitumikia Ufaransa katika mechi tatu kwa dakika zote 90.

Ratiba ya Man United ya pre-season
Jumamosi, Julai 13 - Man United v Perth Glory
Jumatano, Julai 17 - Man United v Leeds
Jumamosi, Julai 20 - Man United v Inter Milan
Alhamisi, Julai 25 - Tottenham v Man United
Jumanne, Julai 30 - Kristiansund v Man United
Jumamosi, Agosti 3 - Man United v AC Milan


EmoticonEmoticon