#SPORTS:Real Madrid Watoa Pesa Na Mchezaji Ili Kumnasa Pogba

Real Madrid wameripotiwa kuweka mezani ofa ya Pauni 72 milioni pamoja na mchezaji mmoja ama Isco au Gareth Bale ili tu wamsajili kiungo Paul Pogba.

Wababe hao wa Bernabeu wanaoonelewa na Zinedine Zidane wamedaiwa kuhitaji sanan huduma ya Pogba na hivyo wanatafuta namna ya kuwashawishi Manchester United ili kufanya biashara hiyo.

Kiungo Pogba, alisema mpango wake wa kutaka kuachana na maisha ya Old Trafford kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, mpango ambao uliungwa mkono na wakala wake, Mino Raiola alipozungumza Ijumaa.
Man United bado wamekuwa wakiweka ngumu kuachana na staa wao huyo ambaye mkataba wake kwa sasa umebakiza miaka mitatu, wakidai kwamba hawataki kumuuza katika dirisha hili la mwaka huu.

Hata hivyo, taarifa za kutoka Hispania zinadai Real Madrid wametafuta namna nzuri ya kuwashawishi wababe hao wa Ligi Kuu England kwa kuwaweka mzigo wa Pauni 72 milioni mezani pamoja na mchezaji mmoja, Isco au Bale na kazi itabaki kwao kuchagua.

Bale anaonekana kama mchezaji wa nyongeza tu huko Bernabeu, wakitaka kumwondoa ili kukwepa kuendelea kumlipa mshahara mkubwa, wakati Isco ndiye mchezaji ambaye anaweza kupata nafasi chini ya kocha Zidane kwa hao waliotajwa kutaka kuwekwa kwenye ofa hiyo ya kubeba Pogba. Man United nao hawana shida na Bale.


EmoticonEmoticon