#SPORTS:Tunisia Yatinga Robo Fainali Afcon 2019, Ivory Cost Kunani...?

Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.
Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.
Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa ziada Rami Bedoui kujifunga kupitia kichwa dakika za lala salama alipogusa mpira kwa mara ya kwanza.

Kwa Upande mwingine Wilfried Zaha alifunga goli la ushindi na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Mali 1-0 ili kutinga robo fainali ya michuano ya Afcon.

Ivory Coast sasa itacheza dhidi ya Algeria katika mechi ya robo fainali siku ya Alhamisi.


EmoticonEmoticon