Tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi,
zinaonesha kuwa ulaji wa ufuta ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa
binadamu.
Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari,
shambulio la moyo, kuimarisha mmeng’enyo wa chakula, huondoa lehemu, huboresha
ngozi, huondoa na kukinga saratani na kuongeza damu. Pia ufuta huzuia mwili
kuharibiwa na mionzi na mionzi ya jua, hulinda ini dhidi ya madhara ya pombe,
hung’arisha ngozi na kuimarisha afya ya macho.
Faida nyingine kuwa ni kuzuia maradhi ya
kinywa. Pia huimarisha mfumo wa upumuaji, lishe kwa watoto wadogo na kuimarisha
afya ya nywele na hivyo kuzuia tatizo la nywele kunyonyoka na kuota nywele kwa
wale wenye uhaba au kutoota nywele.
Hiyo ni kutokana na aina mbalimbali za
virutubisho vilivyomo katika mbegu za ufuta kama vile, protini, mafuta, madini
kadhaa kama ya kopa, kalishiamu (calcium), chuma, zinki, fosforasi, manganizi,
magineziamu na thiamine.
KISUKARI:
Ufuta huzuia na kutibu ugonjwa huo kutokana
na mbegu zake kuwa na madini ya magneziamu ambayo yakiwa mwilini huzuia
visababishi vya sukari kama vile tatizo la insulini na kongosho kutofanya kazi
ipasavyo. Pia mafuta ya ufuta huimarisha kuta za plasma na hatimaye kuwa na
uwezo zaidi wa kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu.
KUKOSA CHOO, SARATANI
Mtu mwenye matatizo ya kukosa choo au choo
kigumu, anapaswa kula kwa wingi ufuta kutokana na virutubisho hivyo kurahisisha
mmeng’enyo wa chakula na kufanya hali hizo kutoweka na kuondokana na tatizo la
ugonjwa wa bawasiri.
Kuhusu ugonjwa wa Saratani, mbegu za ufuta
zina misombo (compounds) kama vile asidi aina ya phytic madini ya maginesiamu
na phytosterols ambayo kwa pamoja huukinga mwili na kuondoa sumusumu zinazosababisha
saratani. Ufuta pia ni tiba ya matatizo yanayokabili kinywa.
Kwa miaka mingi sasa watu wa kabila la
Ayurveda huko barani Asia, wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama tiba na
kinga ya matatizo ya kinywa ikijumuisha meno, fizi na kingo za mdomo au kinywa.
SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA), MATATIZO YA
UZAZI, KUONDOA KITAMBI
Ufuta hutibu pia matatizo ya moyo na
shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambapo mara baada ya kula ufuta
hushuka na kuwa la wastani kwa muda mfupi ikiwa matumizi yake yatazingatiwa.
Ufuta huweza kuimarisha moyo na kuulinda
usishambuliwe na magonjwa ikiwa ni pamoja na kushusha ‘presha’ ya juu kutokana
na virutubisho hivyo.
MATATIZO YA FIGO, KIBOFU.
Ufuta ni tiba muhimu katika tiba ya figo
ikiwemo kuondoa mawe kwenye figo na matatizo ya kibofu. Pia una uwezo wa kutibu
kipindupindu na kuzuia kuhara, kuweka sawa homoni zinazosababisha mzunguko wa
hedhi kwa mwanamke kwenda sawa.
Huongeza nguvu kwenye mifupa na kuimarisha
misuli mwilini kutokana na kirutubisho cha Kalishiamu kilichomo. Huzuia na
kutibu maumivu ya tumbo ya ghafla.
Ufuta pia ni tiba nzuri kwa matatizo ya mfumo
wa upumuaji kwani virutubisho vilivyomo huyakinga mapafu dhidi ya hewa chafu na
magonjwa yanayoambata na kusababisha mfumo wa hewa kutokuwa mzuri.
MATATIZO YA INI NA MACHO
Mtaalamu mwingine wa tiba lishe, Dk. Josh Axe
wa nchini Marekani anasema kupitia kitabu chake cha Eat Dirt kuwa ufuta hulinda
ini dhidi ya magonjwa.
Hiyo ni pamoja na kulifanya ini kuwa na uwezo
wa kufanya kazi ipasavyo na kuliepusha na magonjwa hasa ikiwa limeathiriwa na
pombe kwani ufuta huondoa sumu zilizomo zinazotokana na matumizi ya pombe.
EmoticonEmoticon