#TEKNOJIA:Kosa Kubwa Analolijutia Billionaire Bill Gates

Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates amenukuliwa akisema kuwa katika moja ya kosa lake kubwa la wakati wote alilolifanya ni kuiacha Android kuongoza katika mifumo ya uendeshaji Duniani.
Amesema katika ulimwengu wa programu anayeongoza katika kuwa na programu endeshaji inayotumika kwenye vifaa vingi zaidi ndiye anakuwa mshindi wa masoko yote. Hivyo kwa upande wa Microsoft imefanya kosa kubwa ambalo limeifanya Android kuongoza sokoni.
Android kwa sasa ndio mfumo endeshi unaoongoza kwa kutumiwa na watu wengi zaidi duniani ukifuatiwa na mfumo wa Microsoft, yaani Windows.
Mfumo Wa Android ndyo mfumo ulio na watumiaji wengi duniani kwa wakati huu ukitofautishwa na kipindi cha nyuma ambacho Blackberry ndyo walikuwa wamelishika soko. 
Microsoft ilijaribu kuleta programu endeshaji spesheli kwa ajili ya simu iliyokwenda kwa jina la Windows Mobile kwa upande wa simu zake za Windows Phone lakini haikupokelewa vizuri sokoni na pia kwa watengenezaji wa apps. Microsoft ikajikuta bado inabaki ikitamba katika kompyuta zaidi.


EmoticonEmoticon