App Zitakazofanya Instagram Yako Ijulikane Na Kupata Followers

Instagram
Instagram ni mtandao maarufu sana kwa sasa,kwa mujibu wa tovuti ya Orbelo, hadi mwezi wa tatu mwaka 2019 Instagram Inatumiwa na zaidi ya watu Bilioni 1 kila mwezi, ikiwa ni mtandao wa pili kutumiwa na watu wengi zaidi duniani baada ya mtandao wa Facebook.

Tumekusogezea App zitakazoweza kukusaidia katika akaunti yako ya instagram na kuifanya kuonekana ya kisasa huku ikitambuliwa na watu wengi na kupata wafuasi wengi (followers)

Unfollow For Instagram
App hii ya Unfollow ni app nzuri sana kwa sababu inakupa urahisi wa kufollow watu kwa urahisi na pia ku-unfollow watu kwa haraka, app hii inaweza kusaidia sana kama wewe unataka kupunguza watu kwenye akaunti yako hasa wale ambao hawakufuati (Follow) lakini wewe unawafuata.

Profile Photo Downloader For Instagram
Kama kwa namna yoyote ungependa kuangalia au kudownload picha ya Profile ya mtu yoyote kupitia Instagram basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii itakupa uwezo wa kupakua Profile Picture au picha ya wasifu kwenye akaunti ya mtu yoyote ya Instagram.

Download & Repost for Instagram
Kama unahitaji kudownload picha ya mtu yoyote au unataka kurepost picha ya mtu kwenye akaunti yako ya Instagram basi app hii ni nzuri sana kwako, App hii itakupa uwezo wa ku-repost pamoja na ku-download picha yoyote kwa haraka kabisa.

Tagify
Hashtag ni moja kati ya kitu muhimu sana ambacho kitakusaidia kufikia watu wengi sana kwenye akaunti ya Instagram, kama wewe unayo akaunti ambayo ungependa watu waijue kwa haraka basi hakikisha unatumia hashtags kwenye kila post yako. App hii ya Tagify itakusaidia kuchagua hashtag kulingana na picha unayotaka kupost.

Apphi
Apphi ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya Instagram, App hii itakusaidia kuandaa post na kuziweka zijipost zenyewe baadae, kupitia app hii unaweza kuweka hata post za wiki nzima na zitaweza kujipost zenyewe kila siku.

Unfold
Kama wewe ni mpenzi wa Instagram hasa sehemu ya Stories basi app hii itakusaidia sana, App hii itakusaidia kuweza kutengeneza picha au video nzuri ambazo unaweza kuweka kwenye akaunti yako kupitia sehemu ya Stories.

Canva
App hii ni nzuri sana na itakupa wepesi sana hasa kwenye kutengeneza post zako kwenye akaunti yako ya Instagram. Mbali na Instagram pia utaweza kutengeneza picha au vitu vingine mbalimbali kwa urahisi.

Inshot
Inshot ni moja ya app maarufu sana na bora sana kwa watumiaji wa Instagram, app hii inakupa uwezo wa kufitisha picha pamoja na video na kufanya ziwe na muonekano mzuri kupitia akaunti yako ya Instagram, kama mpaka sasa huna appa hii ni wakati wako kudownload sasa.


EmoticonEmoticon