Mambo 4 Yatakayouwa Betri Ya Simu Yako

Kwenye kuchaji simu ni watu wengu wanafanya makosa mbalimbali ambayo yanasababisha mfumo wa kuchati au ata betri za simu zao kuharibika mapema.

Haya ni Mambo Ambayo yanachangia Betri ya Simu yako kufa mapema.
1 Simu Kuisha Chaji Mpaka 0%
Inashauriwa simu kuchajiwa pindi inapofikisha Aslimia 5% hadi 15%

2.Kuacha Simu Kwenye Chaji Kwa Muda Mrefu
Inashauriwa kutoa simu yako kwenye chaji baada ya kujaa(Hili linawahusu wake wanaolala usiku na kuiacha simu kwenye umeme)


3.Kutumia Charger ambazo sio Original
Inashauriwa kununua simu original kwa maduka yanayoaminikana na kutumia charger maalumu uliyouziwa nayo simu ambayo kampuni husika imefanya vipimo vya umeme kuendana na betri ya simu yako

4.Kuchaji Simu Ikiwa Na Joto Kali
Je simu yako ilikuwa eneo lenye joto kali? Iwe uliisahau eneo la dirishani au kwenye gari na matokeo yake simu kuwa ya moto usiiweke kwenye chaji hadi itakapopoa. Kuweka kwenye chaji na kufanya betri kupata umeme wakati lina joto kutasababisha betri kuanza kupoteza ubora wake.


EmoticonEmoticon