#TEKNOLOJIA:Mtandao Wa Facebook Waathibiwa Na Tume Ya Marekani

Tume ya udhibiti wa masuala ya kibiashara nchini Marekani imeidhinisha faini ya dola bilioni 5 dhidi ya kampuni ya mtandao wa habari wa Facebook kwa ajili ya uchunguzi wa udukuzi wa data binafsi, vinasema vyombo vya habari vya Marekani.
Tume hiyo (FTC) imekuwa ikifanya uchunguzi juu ya madai kwamba taasisi ya ushauri wa kisiasa ya Cambridge Analytica ilipata taarifa kwa njia isiyotakiwa za watumiaji milioni 87wa mtandao wa Facebook.
Malipo hayo yaliiidhinishwa na tume ya FTC kwa kura 3-2, Kelele zimevihahamisha vyombo vya habari vya Marekani.
Facebook na FTC wameiambia BBC kuwa hawana la kuzungumzia juu ya repoti hiyo ya uchunguzi.
Haijafahamika ikiwa Mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg atachukuliwa hatua zaidi kufuatia faini iliyopigwa kampuni yake


EmoticonEmoticon