Fahamu Rangi Ya Bluu Facebook Ina Maana Gani?

Ni wazi ili kufanya mtandao/tovuti kuvutia sana watu, na iwe ya kirafiki zaidi ni lazima rangi izingatiwe sana. 

Wakati Facebook inatengenezwa muanzilishi wake rangi ambayo alikuwa nayo katika akili yake ilikua ni rangi ya bluu.
Rangi ya bluu ina maana ya Amani hili lina maana kubwa sana kwani kumbuka kazi kubwa ya mtandao huo wa kijamii ni kuunganisha dunia nzima katika mawasiliano.

Rangi ya bluu inaonyesha hadhi ya utulivu na ni moja kati ya rangi bora kabisa dunaini. Sifa za rangi hii ndizo pekee ambazo zimemfanya muanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg  kuichagua  rangi hii.

Tangu Facebook ianzishwe 2004 mpaka leo ni vipengele vingi sana vimebadilika lakini katika swala la rangi hawajagusa kabisa, hivyo basi hakuna mabadiliko yoyote juu ya hilo.

Muanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg  alinukuliwa akisema “BLUE IS THE RICHEST COLOR FOR ME – I CAN SEE ALL OF BLUE”.


EmoticonEmoticon