Timu Tano Za Kuangalia Kwenye UEFA Ligi Msimu Ujao

Dirisha la Uhamisho wa wachezaji limefunguliwa na hivyo vilabu kadhaa zinaangazia kununua wachezaji wapya kuvisuka vilabu vyao upya.

Mashabiki wa soka duniani kote watayaelekeza macho yao kwa vilabu kadhaa ili kuwaaangazia wachezaji fulani ama kuangazia hali fulani.

1.Barcelona
Barcelona imewasajili wakali watatu kufikia sasa huku ikitumia kima cha millioni mia mbili. Baada ya ujio wake Antoinne Griezmann, Barcelona huenda ikamsajili Neymar kutoka Paris Saint Germain ya ufaransa.
Mastaa hawa watakuwa jambo la kupendeza sana kuwatazama wakicheza pamoja kuona iwapo wanauwezo wa kurudisha taji la klabu bingwa barani ulaya ugani Camp Nou.

2.Juventus
Mathias De light alikataa kusajili mkataba na Barcelona kisha akajiunga na Juventus kwa madai kuwa waitaliano hao walikuwa na mipango mizuri ikilinganishwa na Barcelona.
Uwepo wake Cristiano Ronaldo pamoja na ujio wake Maurizio Sarri unaifanya Juventus iwe moja kati ya timu hatari zaidi msimu ujao katika ligi ya mabingwa barani ulaya.

3.Liverpool
Bila shaka lazima tumwangazie bingwa mtetezi wa taji hili Liverpool. Jurgen Klopp huenda asufanye usajili wowote msimu huu kwani kikosi chake  kiko tisti kabisa. Liverpool itakuwa inatarajia kulitetea taji lao kama walivyio fanya Real Madrid.

4.Manchester City
Pep Gurdiola kwa sasa anakisuka kikosi chake upya kwa ajili ya mechi za klabu bingwa barani ulaya pamoja na mechi za  ligi kuu nchini Uingereza.
Guardiola kwa sasa matamanio yake ni ligi ya mabingwa barani  ulaya ila sio ligi kuu. Manchester City ilibanduliwa na Totenham Hotspurs msimu uliopita kwenye awamu ya robo fainali huku raudi hii ikitarajia kuwa Gurdiola yupo tayari kubishana na wakali kama Barcelona.

5.Real Madrid
Eden Hazard anatarajiwa kuondoa uzuni wa mashabiki wa Real Madrid  msimu ujao. Madrid ilibanduliwa  kimadharau na Ajax baada ya kugaragazwa magoli manne bila kwa moja ugani Santiago Bernabue. Madrid kwa  sasa imewasajili Luka Jovic, Eden Hazard pamoja na Mendy ilikuwasaidia kurudisha taji la UEFA ugani Santiago Bernabue.


EmoticonEmoticon