Umeshaziona Nguo Zenye Air Condition(Kiyoyozi)?China Wameleta Hii


Tumezoea kuona vifaa vya kupooza hewa – yaani AC kuwa kwenye majumba, magari na maofisini. Fikiria ya kuweza kutembea nayo popote? Sony waja na kipooza kitakachowekwa ndani ya nguo yako.
Fikiria unatamani kuvaa suti kwenda kwenye shughuli ya kikazi lakini hali ya hewa hairuhusu, yaani joto ni kali. Hapa ndio teknolojia mpya kutoka Sony inalenga kutatua, nguo yako iwe na kipooza (AC) ndani yake.

Kupitia kitengo chake cha teknolojia za majaribio na zinazokusanyiwa mitaji kupitia mfumo wa uchangiaji kwa wale wanaotaka kununua bidhaa kwa mara ya kwanza (crowdfunding) wamekuja na bidhaa ya kitofauti sana waliyoipa jina la The Reon Pocket.

Mfumo huo wa kipooza cha kwenye nguo upo kihivi;
1.Kuna mashati spesheli yatakayokuwa na kama kimfuko kidogo eneo la mgongoni chini kidogo ya shingo.
2.Kupitia kifaa kidogo hicho kitaweza kukaa na chaji ndani ya masaa 24 kwa kuchaji mara moja tuu – kwa muda wa masaa mawili.
3.Kupitia app utakayoweza kuweka kwenye simu yako utaweza kupooza joto lako kwa digrii 4 (C) chini na pia kama kuna baridi sana basi utaweza kuongeza joto kwa kiasi takribani digrii 2 zaidi.
Lengo la Sony ni kuwezesha baadae app hiyo kuwa na uwezo wa kuweka mpangilio (setting) wa kusimamia kiwango cha joto bila uhitaji wa wewe kufanya chochote, yaani ‘automatically’.


EmoticonEmoticon