Wanawake Wajawazito Wenye Kisukari, Inawapasa Kuripoti Katika Kliniki Zao Mapema

Wanawake wenye ugonjwa wa kisukari wana uwezekano mara nne wa kujifungua watoto njiti na hivyo kutoweza kuishi kuliko wasio na ugonjwa huo , umebaini utafiti
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Glasgow waliangalia rekodi za karibu wanawake 4,000 wa Uskochi wenye ugonjwa wa kisukari.
Walibaini kuwa viwango vya juu vya sukari mwilini miongoni mwa wanawake wajawazito wenye maradhi ya kisukari walikuwa na "uwezekano wa hatari " ya kupata watoto njiti.
Kiwango cha unene wa mwili (BMI) cha mwanamke mwenye ugonjwa wa kisukari pia ni sababu kubwa, utafiti ulibaini.
Watafiti pia walibaini kuwa theluthi tatu ya watoto wa aina hiyo wanaozaliwa kwa wanawake wenye ugonjwa wa kisukari hutokea wanapomaliza muhula kamili.
Dr Sharon Mackin, ambaye alifanya utafiti huo, amesema kuwa: "Ni muhimu kwamba sisi kama wataalamu wa huduma ya afya , tutafute njia bora za kuwasaidia wanawake wakati wanapokuwa na umri wa kupata ujauzito kudhibiti uzito wao na viwango vya sukari mwilini, ili wanapokuwa wajawazito iwe kwa kupanga au kwa kutopanga , wawe wamejiandaa na kupunguza hatari za matokeo mabaya.
"Ni muhimu kwa wanawake wenye kisukari wawe watu wenye kujali hili, na wawe na uwezo wa kupata ushauri nasaha wa awali kabla ya kupata ujauzito, hata kama ikiwezekana wapange ujauzito.
"Wanawake wenye ugonjwa kisukari pia wanapaswa kuwasiliana na kliniki zao za kisukari mapema iwezekanavyo mara wanapotambua kuwa ni wajawazito ili tuweze kuwaona na kuwasaidia mapema ."
Utafiti ulibaini kuwa kujifungua mapema kunaweza kuangaliwa kama "chaguo linalowavutia wengi " lakini kwamba utafiti zaidi unahitajika kabla ya kuidhinisha hilo kwa kuwa muda wa kujifungua mapema unatakiwa kupangwa.
Dr Mackin amesema kuwa swali la kujiuliza "linapaswa kuwa ni ikiwa kujifungua mapema kwa wanawake wote wajawazito wenye ugonjwa wa kisukari kunaweza kuwazuwia kujifungua watoto njiti ".
Amesema: "hatufahamu jibu kuhusu hili . Muda sahihi wa kujifungua wa nujauzito wa aina hiyo haujulikani."
Utafiti ulibaini kuwa watoto wachanga 5,392 walizaliwa kwa akina mama 3,847 wenye kisukari katika Uskochi mwenzi Aprili 1998 hadi Juni 2016.


EmoticonEmoticon