Alichokisema Kocha Wa Arsenal Kuhusiana na Mesut Ozil Na Sead Kolasinac

Kocha wa Arsenal Unai Emery ana uhakika asilimia mia moja kuwa wachezaji wake Mesut Ozil na Sead Kolasinac wako tayari kurejea katika kikosi chake, baada ya kuwachwa nje ya mechi ya kwanza ya ligi ya EPL dhidi ya Newcastle kutokana na usalama wao.
Wawili hao walikua wamehusika na jaribio la kuibiwa na watu wawili ambao walitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. Emery pia anadai wawili hao wako katika hali nzuri ya kimawazo na watafanya vyema.


EmoticonEmoticon