Chanjo Dhidi Ya Ugonjwa Huu wa zinaa Yapita


Chanjo ya kuwakinga watu dhidi ya magonjwa ya zinaa imepita uchunguzi wa kwanza wa kiusalama.
Ni ya kwanza kupita majaribio kwa binadamu.
Wataalamu wanasema chanjo hiyo ndio njia bora ya kukabiliana na ugonjwa wa Chlamydia ambao unachangia karibu ya nusu ya maambukizi ya magonjwa yote ya zinaa Uingereza.
Uchunguzi zaidi unapendekezwa kufanywa ili kubaini jinsi chanjo hiyo inavyofanya kazi na itolewe kwa kiwango gani, linasema jarida la Lancet la magonjwa ya kuambukiza.
Majaribio hayo yatachukua miaka kadhaa kubainishwa lakini kwa sasa wataalamu wanapendekeza njia bora zaidi ya kijikinga na maambukizi ya chlamydia ni kutumia mipira ya kondomu.

Chlamydia ni nini?
Ni ugonjwa uanaoambukizwa kupitia bakteria inayomuingia mtu anayefanya ngono bila kinga( hata bila kumuingilia mtu).
Bakteria ya Chlamydia huishi katika mazingira ya maji maji inayopatikana kwenye manii ya wanaume na katika sehemu ya siri ya mwanamke.
Mara nyingi mtu aliyeambukizwa haoneshi dalili zozote na dio sababu watu huutaja ugonjwa huo kuwa ugonjwa wa "siri".
Usipotibiwa kwa kutumia antibiotiki, unaweza kusababisha madhara makubwa yatakayathiri kizazi cha muathiriwa.
Watu walio chini ya miaka 25 ambao wanapendelea kufanya ngono wanashauriwa kufanya vipimo vya chlamydia kila mwaka.
Huduma ya afya ya kitaifa NHS nchini Uingereza inatoa huduma ya uchunguzi bila malipo.
Watu pia wanaweza kujifanyia uchungizi binafsi kwa kununua vifaa maalum vilivyoidhinishwa kutoka kwa maduka ya kuuza dawa.

Kwanini chanjo hii ni uhimu?
Japo antibiotiki inaweza kutibu chlamydia, mtu anaweza kupata mambukizi mapya akiingiliana kimapenzi na mtu aliye na ugonjwa huo.
Chlamydia inasalia kuwa ugonjwa wa zinaa ambao maabukizi yake yapo juu zaidi licha ya kuwa na tiba.
Chanjo huenda ikatoa ulinzi wa muda mrefu, wataalamu wana tumai.
Katika awamu ya majaribio , watafiti kutoka Taasisi ya Imperial mjini London walilinganisha dawa mbili tofauti na kuwadunga wanawake 35.
Dawa zote zilionekana kuwa salama, lakini moja ilikuwa na nguvu zaidi.
Watafiti sasa wanataka kuweka chanjo hiyo katika awamu nyingine ya majaribio.
Mchunguzi Prof Robin Shattock alisema: "Matokea yalikua ya kuridhisha kwa sababu inaonesha chanjo hii ni salama na inatoa ulinzi ambao huenda ukakabiliana na maambukizi dhidi ya ugonjwa wa chlamydia.
"Awamu inayofuata ni kuendeleza mbele chanjo hii kwa kuifanyia uchunguzi zaidi, hadi hilo lifanyike, hatuwezi kubaini ikiwa inaweza kutoa kutoa ulinzi au la.
"Tunatarajia kuanza awamu ya pili ya majaribio katika kipindi cha mwaka mmoja au miwili ijayo.
Majaribio hayo yakienda kama ilivyopangwa huenda tukabuni chanjo ambayo itazinduliwa katika kitika kipindi cha miaka mitano ijayo."
Alipendekeza chanjo hiyo ipeanwe pamoja na sindano ya HPV jambaya sasa inatumiawa kujikinga dhidi ya saratani ya shingio ya uzazi.
Msemaji kutoka kundi la vijana la Brook linaloangazia masuala ya afya ya uzazi anasema: "Kwa kweli matokeo ya majaribio ya awali yanatia moyo sana, japo ni mapema mno kuzungumzia ufanisi wake lakini tunaelekea kupata chanjo thabiti itakayotoa kinga imara miaka ijayo.


EmoticonEmoticon