David Luiz Ataka Kuhamia Arsenal iLa Chelsea Hawataki Kumwachia

Mlinzi wa Chelsea David Luiz anataka kuhamia Arsenal. Kiuongo huyo wa The Blues alifanya mazoezi mbali na kikosi cha Frank Lampard jana. 
Kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery anasema anataka kumsajili kiungo wa kati kabla ya makataa ya leo na inaaminika kuwa Luiz yupo kwenye orodha yake, ingawaje hajawasilisha ofa rasmi ya kumtaka.
Chelsea hawataki kumwachilia Luiz kwenda Arsenal kutokana na marufuku yao ya kusajili wachezaji wapya hadi msimu ujao wa joto.
Hayo yakijiri, DC United wanajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, wanapojaribu kujaza pengo lililoachwa wazi na Wayne Rooney anayeelekea Derby.


EmoticonEmoticon